Polisi Nchini Kenya, wanaendelea kuimarisha usalama nje ya majengo ya Bunge la Kitaifa kwa kufunga barabara zote zinazoelekea eneo hilo, huku hoja ya kumuondoa madarakani Naibu wa Rais Rigathi Gachagua ikipokelewa kwa ajili ya kujadiliwa kwa madai amekiuka katiba ya nchi.

Maelezo ya kuwasilishwa kwa hoja hiyo, yametolewa na Spika wa Bunge la Kenya, Moses Wetangula wakati ambapo Vyombo vya Habari vya Kenya vikiripoti kuwa Makamu huyo wa rais ametofautiana na Rais William Ruto.

Spika wa Bunge la Kitaifa wa Kenya, Moses Wetangula.

Tayari zaidi ya theluthi moja ya wabunge wamesaini hoja hiyo iliyowasilishwa na Mbunge Mwengi Mutuse kutoka kambi ya muungano wa Ruto, wakimtuhumu Gachagua kwamba anawanyima watu fursa za kupata uteuzi wa nafasi za umma na rasilimali.

Naibu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Rigathi Gachagua.

Mpasuko kati ya Ruto na Gachagua umekuwa ukionekana wazi katika siku za hivi karibuni, huku Makamu huyo wa Rais akisema ametengwa katika shughuli za kiserikali na Wetangula akionesha kuunga mkono jambo hilo kwa kusema suala la kuwabagua wakenya kikabila na kimaeneo ni kinyume cha sheria.

Dkt. Biteko: Wasomesheni Watoto kuchochea maendeleo
EWURA yatangaza ahueni bei kikomo za Mafuta