Mgombea uraisi wa upinzani nchini Tunisia, Ayachi Zammel amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela baada ya kutiwa hatiani kwenye mashitaka manne, likiwemo la kughushi kura.
Hata hivyo, Wakili wa mgombea huyo amesema licha ya hukumu hiyo bado Zammel anabakia kuwa mgombea halali katika uchaguzi huo wa rais unaotarajia kufanyika Oktoba 6, 2024.
Zammel ambaye ni Mbunge wa zamani na mfanyabiashara, anaongoza chama chake chenye sera ya ukombozi na amekuwa ni mmoja kati ya wagombea wawili walioidhinishwa na Tume ya Uchaguzi ya Tunisia, kupambana na Rais Kais Saed.
Hata hivyo, Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo pia imewazuia Wagombea wengine 14 kuwania nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi huo, kutokana na tuhuma kadhaa.