Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka wazazi na walezi nchini kutumia fursa ya miundombinu ya shule inayojengwa kwa ushirikiano wa Serikali na wafadhili, kuwasomesha Watoto ili kuchochea maendeleo.
Dkt. Biteko amesema hayo wakati akizindua miundombinu ya Shule ya Sekondari ya Milles and Kimbery White iliyojengwa kwa zaidi ya shilingi Bilioni 12 Wilayani Mkinga kwa lengo la kuwawezesha Watoto wa eneo hili kujikwamua katika ya elimu.
Pia amewataka wanafunzi kutumia nafasi wanayoipata kujiendeleza kwa kujisomea na kujenga uelewa huku wakichukua tahadhari dhidi ya baadhi ya maudhui yanayopatikana katika mitandao ya kijamii kwa kufanya hivyo hawatajuta kutokana na matokeo mazuri watakayoyapata.
Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda amesema Wizara yake imejipanga kuanzisha mafunzo ya amali ambapo shule zaidi ya 100 zitajengwa nchi nzima ili kuwawezesha wanafunzi wahitimu elimu wakiwa na ujuzi.
Naye Mtendaji wa Mkuu wa ABBOTT, Robert Ford amesema ujenzi wa shule hiyo unakusudia kuwasaidia Watoto katika eneo hilo kupata elimu na ujuzi huku akiwashukuru wakazi wa eneo la Mapatano kwa ushirikiano walionesha katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi.

Mbinu iliyowasaidia wengi kufaulu mitihani ya Chuo
Hoja ya kumng'oa Mkamu wa Rais: Ulinzi waimarishwa nje ya Bunge