Mkuu wa Majeshi ya Iran, Meja Jenerali Mohammad Bagheri ametishia kulenga miundombinu ya Israel, ikiwa itachukua hatua zozote za kulipiza kisasi dhidi ya Tehran, huku akilitaka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, kitengo cha kijeshi tayari kujilinda na operesheni kurudia shambulio.
Hta ahivyo, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu tayari ameahidi kuwa Iran itakabiliwa na matokeo makubwa kwa shambulio hilo huku vikosi vya ziada vikijiunga na mashambulio machache ya ndani yaliyoelekezwa huko Hezbollah, kusini mwa Lebanon.
Awali, Hezbollah ilisema ilizuia shambulio la ardhini la Israeli katika kijiji cha mpakani cha kusini mwa Lebanon, huku jeshi la Israeli likiwa halijazungumza chochote kuhusiana na tukio hilo.
Hatua hiyo, huenda ikasababisha kupanda kwa bei ya mafuta baada ya Iran kurusha makombora ya balistiki dhidi ya Israel na kuzua hofu ya mzozo mkubwa katika eneo la Mashariki ya Kati ambao unaweza kuvuruga usambazaji wa mafuta na Wafanyabiashara wakihofia kwamba kuongezeka kwa mzozo wa kijeshi katika eneo hilo kunaweza kuathiri usafiri wa meli kupitia Mlango-Bahari Hormuz.