Balozi wa Iran wa Umoja wa Mataifa, Danny Danon ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa madhumuni ya nchi yake kurusha makombora karibu 200 Israel, yalilenga kuizuia Israel kutoendelea na mashambulizi.
Danon amesema hatua ya Iran kuishambulia Israel ni kitendo cha uchokozi na iwapo Iran haitozuiliwa basi wimbi jengine la makombora halitoilenga tu Israel bali pia na mataifa mengine hivyo kuziingiza nchi katika mzozo nkubwa utakaoleta madhara kwa raia wasio na hatia.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameapa kulipiza kisasi kutokana na mashambulizi hayo ya Iran huku Iran kupitia kwa Rais Masoud Pezeshkian ikitishia kuwa itajibu vikali zaidi iwapo Israel itathubutu kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi.
Hata hivyo, Jeshi la Israel limetoa amri ya kuwataka watu kuondoka katika maeneo yaliyo na idadi kubwa ya watu ya kusini mwa Beirut huko Lebanon, ikisema itayashambulia maeneo ya Wanamgambo wa Hezbollah, baada ya kiapo hicho cha kisasi cha Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.