Mtendaji Mkuu, wa Shirika la Abbot Fund, Robert Ford, amesema ameridhidhishwa na utekelezaji wa mradi wa maabara ya ujuzi ya Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), huku akiahidi kuwa wataendeleza.
Ford amesema, “hii ni Hospitali namba moja hapa Dodoma. Inabidi mjivunie kuwa na kuwa na hii Hospitali,” amesema C.E.O wa Abbot Fund wakati wa ziara yake BMH.
Shirika hilo liligharamia ujenzi wa maabara ya ujuzi ya Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kwa thamani ya 400m/-. Maabara hii imezinduliwa na Waziri wa Afya, Jenista Mhagama Septemba, 2024.
Kwa upande, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali, Dkt Kessy Shija, amesema ujenzi wa Maabara ya Ujuzi umeanza mwishoni mwa mwaka jana.
“Mradi wa Maabara ya Ujuzi umekamilika mwanzoni mwa mwaka huu na tumekabidhiwa mwezi Machi,” amesema Dkt. Shija kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Prof Abel Makubi.
Dkt. Shija amesema Maabara hii ya Ujuzi itakuwa na manufaa sana kwa watumishi wa Afya kutoka idara za huduma ya dharura.
“Washiriki ishirini wataweza wataweza kushiriki mafunzo kwa awamu moja. Kituo kitakuwa na manufaa sana kwa watumishi wa Afya kutoka idara ya dharura,” amesema Dkt Shija.