Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba amesema moja ya nyenzo muhimu katika kuondoa umasikini kwa watu, ni uwepo wa huduma za Hifadhi ya Jamii.
Mshomba ameyasemwa katika kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari ambapo amesisitiza kuwa, hifadhi ya jamii ni moja ya nguzo kuu ya kuondoa umasikini, hivyo watu waliopo katika sekta rasmi na sekta isiyo rasmi ni muhimu kuhakikisha wanakuwa wanachama wa NSSF.
Vilevile Mshomba ameipongeza Serikali kwa mchango wake mkubwa uliochangia mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha takribani miaka minne, ambayo ni pamoja na ongezeko la thamani ya Mfuko kutoka shilingi 4.8 mwaka 2021 hadi kufikia shilingi trilioni 8.5 hivi sasa sawa na ukuaji wa zaidi ya asilimia 70.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Omar Mziya amesema madhumuni ya kuanzishwa kwa Skimu ya Sekta Binafsi ni pamoja na uongeza wigo wa Hifadhi ya Jamii kwa makundi ambayo hayanufaiki na huduma zao ingawa wanashiriki kikamilifu kuchangia uchumi wa nchi, kusaidia juhudi za serikali za kupunguza umaskini wa kipato kwa wananchi.
Naye Meneja Mifumo wa NSSF, Mihayo Mathayo amesema Mfuko huo unaendelea kuboresha mifumo yake ya TEHAMA, ili kuhakikisha wanachama na wadau wanapata huduma kuirahisi, ambapo hadi sasa huduma na shughuli za NSSF zinafanyika kupitia mifumo kwa kiwango cha asilimia 82.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile akiipongeza NSSF kwa kazi nzuri na uwekezaji wanaofanya ambao una tija kwa jamii na Taifa na kwa kufanya maboresho makubwa katika utendaji kazi ikiwemo kwenye matumizi ya TEHAMA katika kutoa huduma.
Vilevile ametoa wito kwa Wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwa wakati jambo ambalo linawezekana, huku baadhi ya wahariri ambao wastaafu wanufaika wa pensheni ya uzee wakieleza namna mafao hayo wanavyolipwa yanavyo wasaidia.