Sina shaka utakuwa unafahamu ama kusikia kuhusu kuhusu ‘The Tianmen Glass Walkways’ iliyopo kwenye Mlima wa Tianmen Mkoa wa Hunan, Nchini Uchina.

Hiki ni kivutio cha utalii cha kuvutia na chenye changamoto kwa wageni kikiwa na njia za kutembea ambazo hutoa uzoefu wa kipekee kwa kuwaruhusu wageni kutembea kwenye njia zilizosimamishwa za mwinuko wa juu.

Kuna sakafu ya glasi inayoangaza kwa upande wa pili ikionesha mitazamo ya kuvutia na ya kutatanisha ya mandhari ya milima kwa chini.

Njia hizi za glasi, zinazojulikana kama “Skywalks” ziko kwenye miamba na kufanya watu kutoa maoni yoa kuzihusu na hata mazingira yanayozunguka.

Ukipita mahala hapo utaona mabonde ya kina, milima na Barabara ambapo njia yake hiyo ya kutembea kwa kawaida huwa zaidi ya mita 1,400 juu ya usawa wa bahari.

Hii inajumuisha kipengele cha adrenaline kwenye uzoefu na kufanya Wageni wanaothubutu kutembea juu yake kufurahia mchanganyiko wa msisimko na mshangao.

Wengi wao huwa wanatathmini uhandisi wa kuvutia uliowezesha ujenzi wa miundo hiyo katika mazingira magumu kama hayo kiasi cha kuishia kupongeza wahusika.

Ni njia maarufu zaidi ikiwa na urefu wa mita 60, inayojulikana kama “Crystal Dragon Walkway” kutembea katika njia hizo kunahitaji ushujaa na uangalifu maana pana mwendo kidogo, lakini hisia za kipekee za ujasiri hupelekea ushindi.

Vipi ndugu yangu! Wewe unaweza kulifikia eneo hilo na ukatamba kabisa bila hofu kuyafikia mafanikio ya matembezi juu ya mlima kwa kupita njia ya Vioo? jibu kaa nalo kama huna uthubutu au kama si shujaa.

Как использовать индикатор ATR в трейдинге: советы и примеры
Ushirikiano, ubunifu kuliendeleza bara la Afrika - Dkt. Tulia