Ripoti kutoka Nchini Kenya zinasema Naibu Rais wa nchi hiyo, Rigathi Gachagua  amewasilisha ombi katika Mahakama mjini Nairobi akitaka kusitishwa kwa mchakato wa kumuondoa katika nafasi yake, uliowasilishwa na Wabunge mapema wiki hii.

Katika ombo lake kwa Mahakama, Gachagua amesema hoja ya kumshtaki ilikuwa ni ya  uchochezi wa kisiasa uliopangwa, ili kushinda utashi wa uhuru wa watu wa Kenya, uliooneshwa kwenye uchaguzi wa urais wa Agosti 2022.

Naibu huyo wa Rais wa Kenya, amekuwa akikabiliwa na tuhuma mbalimbali, ikiwemo ukosefu wa nidhamu na kumhujumu mkuu wake Rais William Ruto.

Tuhuma zingine ni kuchochea chuki za kikabila na kudhoofisha Serikali na kwamba alihusika na vurugu maandamano ya vijana maarufu Gen Z dhidi ya serikali mapema mwaka huu, madai ambayo ameyakanusha.

Wadau wa lishe watumie vizuri matokeo ya ripoti - Majaliwa
Dkt. Magembe: Shughulikieni changamoto kwenye maeneo yenu