Wakati hali ya usalama ikiwa tete katika eneo la Mashariki ya kati, Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un naye ametishia kutumia silaha za Nyuklia, ili kuisambaratisha Korea Kusini, iwapo nchi hiyo italeta uchokozi kwa Taifa lake.

Taarifa iliyotolewa na Vyombo vya Habari nchini humo, imeeleza kuwa onyo hilo limekuja baada ya Kiongozi wa Korea Kusini kumuonya Kim kwamba ataangushwa iwapo atathubutu kutumia zana za nyuklia.

 

Amesema, “iwapo Korea Kusini itajaribu kutumia jeshi kuingilia uhuru wa Korea Kaskazini, hali kama hiyo ikitokea, Seoul na Jamhuri ya Korea zitaangamia.”

Hata hivyo, majibizano baina ya mataifa hayo mawili si jambo geni, ingawa yanakuja wakati ambao uhasama baina ya mataifa hayo mawili ukizidi kupamba moto.

Tangu mwaka 2022, Kim mara kwa mara amekuwa akitishia kutumia silaha za nyuklia, huku ikidaiwa kuwa hakuna uwezekano wa kutumia silaha hizo, kwani Jeshi la Korea Kaskazini ni dogo.

Tumeimarisha mifumo ukusanyaji wa Mapato - Rais Samia
Vifo watu 278: Mamlaka usafiri wa majini zatupiwa lawama