Anaitwa Yemisi Iranloye, yeye ni Mjasiriamali raia wa Nigeria ambaye amekuwa “Malkia wa Mihogo” asiye na shaka akijipatia pesa nyingi kwa kutumia Kilimo cha Mihogo, licha ya kukabiliwa na ushindani kutoka kwa mashirika ya kimataifa Kibiashara.

Anamiliki Kampuni inayoitwa Psaltry International, akizalisha Tani 10,000 za muhogo kila mwaka, huku mauzo yake ya kila mwaka yakiwa ni Dola 12 milioni.

Mafanikio yake ni uthibitisho wa azimio lake lisiloyumba kibiashara na alianza kilimo hicho katika mji aliozaliwa wa Ilesa, Jimbo la Osun, Nigeria kwa uwekezaji wa kawaida na ufahamu wa kina wa mnyororo wa thamani wa muhogo.

 

Kwa miaka mingi sasa, ameongeza shughuli zake na sasa anamiliki viwanda kadhaa vya kusindika muhogo huku akitoa ajira kwa mamia ya Wanigeria huku akishiriki kikamilifu kukuza mbinu za Kilimo kwa kuwawezesha Wanawake.

Licha ya changamoto zinazowakabili wajasiriamali wa kike nchini Nigeria, Iranloye amevumilia na kuwa mfano wa kuigwa kwa wanaotaka kuwa wafanyabiashara kwa kuwapa msukumo wote wanaojitahidi kuleta mabadiliko katika jamii.

Dkt. Samia: Tutajenga mfumo wa Kodi unaotenda haki
Tumeimarisha mifumo ukusanyaji wa Mapato - Rais Samia