Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amewaonya baadhi ya viongozi wa Serikali wanaowashawishi na kutaka kuwaondoa wananchi wanaoishi maeneo ya malisho, ambayo Serikali ilisharidhia na kutoa tangazo kuruhusu waendelee kuishi.

Mchengerwa ametoa maagizo hayo katika ziara yake katika Halmashauri ya Jiji la Arusha na kuzitaja wilaya za Arumeru, Monduli, Karatu, Longido na Ngorongoro kuwa kuna baadhi yao wamekuwa wakiwashawishi na kutaka kuwaondoa wananchi katika maeneo hayo wakidai yanapimwa kwa ajili ya matumizi mengine.

Amesema, “nasikia kuna michakato wa kuwaondoa wale wananchi kwenye maeneo ya malisho mnaendelea na taratibu za kuwaondoa,kuwashahishi wengine mnatumia mpaka sauti ya Rais kwamba ametaka waondoke huko ni kumchongisha Rais na wananchi,nawaelekeza wakuu wa wilaya nisisikie kiongozi yoyote wa Serikali za Mitaa anawaondoa wananchi.”

Waziri Mchengerwa ameongeza kuwa,  amesikia kwenye baadhi ya maeneo mkoa wa Arusha kuna mchakato wa kuwaondoa wananchi kwenye maeneo hayo huku wengine wakiwashawishi na kutumia sauti ya Rais kwamba anawataka waondoke kwenye maeneo hayo wakati siyo kweli.

“Hakuna mtu mwingine mwenye mamlaka ya kuwaondoa wananchi mpaka pale mipaka hiyo itakaporekebishwa na Waziri wa Tamisemi,maeneo hayo tumeridhia wananchi wapige kura,bahati nzuri GN tumesoma hapa Arusha,” alisema.

Aidha, emuagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kusimamia wilaya hizo na kuwa Serikali ilishatangaza GN na maeneo hayo mchakato wa uchaguzi unaendelea ikiwemo kujiandikisha.

Alisema, Serikali haitasita kumchukulia hatua kiongozi yoyote atakayehusika na mchakato wa kuwaondoka wananchi wanaoishi katika maeneo ya malisho.

Dkt. Mzuri: Waandishi mripoti Habari za Tabianchi
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 6, 2024