Bondia Issa Nampepeche ameondoka na kitita cha Shilingi Milioni tatu baada ya kushinda kwa Knockout ndani ya sekunde ya 40 katika raundi ya kwanza dhidi ya mpinzani Joseph Masunga.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa pamoja na viongozi mbalimbali na mashabiki wa ndondi walifuatilia mapambano yaliyokuwa yakiendelea kwenye ukumbi wa City Centra Hall Magomeni Jijini Dar Es Salaam.

Usiku wa KNOCKOUT YA MAMA uliwakutanisha mabondia kutoka nchi za Ghana, Uganda, South African, Tanzania na Angola wanatarajia kuchuana katika usiku huu.

Bondia wa Tanzania Said Mohamed alicheza Pambano la IBA Intercontinental dhidi ya mpinzania wake Lusanda Komanisa wa africa kusini juku Ibrahim Mustafa akicheza pambano la WBC Africa dhidi ya Ecoch Tettey wa Ghana.

#KnockoutyaMAMA

 

#KnockoutyaMAMA

Pointi zampa Mchanja Milioni 1.5 za Knockout ya Mama
Picha: Matukio ya utangulizi #Knockoutyamama