Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga ameendelea na ziara yake ya kikazi Katika wilaya ya Kiteto na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya afya, elimu, barabara, maji na umeme katika kata za Ndirigishi, Matui, Engusero, Chapakazi, Kaloleni na Kibaya.

Akiwa katika kata ya Ndirigishi RC Sendiga, amekagua ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika shule ya Sekondari inayojengwa kwa zaidi ya Shilingi milioni 400. Akiwa shuleni hapo ameagiza majengo ambayo hayajakamilika yakamilishwe kwa wakati ikiwemo mabweni 2, Nyumba ya Mwalimu, Madarasa msanne na vyoo.

Sambamba na hilo RC Sendiga ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kufanya msawazo wa watumishi hasa katika sekta ya elimu ili kuboresha upatikanaji wa elimu bora kwa shule zenye upungufu wa walimu.

Aidha, Sendiga amekagua ujenzi wa Ghala la mazao kata ya Engusero na kumuagiza mkandarasi kurudi eneo la mradi na kufanya marekebisho kwenye maeneo yaliyobainika kuwa na mapungufu, huku akiiagiza NFRA kulipa wakulima wenye madai ifikapo kesho asubuhi Oktoba 8, 2024.

Afya: Hii hapa Tiba ya ukweli ugonjwa wa Kifua Kikuu
Matengenezo ya Barabara: TARURA yawapa somo Sierra Leone