Johansen Buberwa – Kagera.

Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA, Mkoa wa Kagera imewataka Wafanyabishara kutoa taarifa juu ya wakwepa kodi wanaoingiza bidhaa zao kwa njia za magendo, jambo ambalo linaweza kuleta athali kwenye Taifa.

Rai hiyo imetolewa na Afisa elimu na mawasiliano kwa Umma, Rwekaza Rwegoshora wakati kizungumza na baadhi ya Wajasiliamali na Wafanyabishara katika semina ya siku moja kwenye wiki ya mtoa huduma kwa wateja, Manispaa ya Bukoba.

Amesema, kutokana na mkoa huo kuwa karibu na nchi za Afrika mashariki kuna maeneo ambayo sio rasmi yanayotumiwa na Watu wasio wema wazuri kupitisha magendo yao, hali inayopelekea Serikali kukosa mapato huku bidhaa zinazoingizwa nchini zikiwa hazijathibitishwa ubora na hivyo kuweza kuleta athari kwa watumiaji.

Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Kagera, Castro John amesema kwasasa wanaendelea kutoa elimu kwa Wafanyabishara wote wa mkoa huo juu ya namna ya kukuza pamoja mapato na kurasimisha Biashara zao.

Hata hivyo, ametumia furusa hiyo kuwasisitiza Wafanyabishara kutoa risiti halali kwa wateja wanaowahudumia, kwani  muuzaji na mnunuzi watakuwa na makosa kisheria wasipofanya hivyo na ikithibitika atatozwa faini.

Nao baadhi wa Wafanyabishara kutoa Mkoani humo akiwemo Ismail Ibrahimu wameishukuru TRA kwa kuwapatia semina na kuwakumbusha wajibu wao, huku wakiahidi kuendelea kutoa ushirikiano.

Mpanda: TAA yarudisha Shukrani kwa Jamii
Mwizi wa Saa: Hata mimi nilifumba Macho kama wewe - Mwallimu