Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Wananchi wametakiwa kushiriki katika maadhimisho ya siku ya Mbolea Duniani yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Manyara Oktoba 10 – 13, 2024 huku yakitarajia kuwaunganisha Wakulima na Wazalishaji wa Mbolea pamoja na pembejeo za Kilimo.

Akizungumza na Wanahabari, Mkuu wa Mkoa waMmanyara, Queen Sendiga amesema lengo la maadhimisho hayo ni kutoa elimu kwa Wananchi juu ya matumizi Bora ya mbolea na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Kilimo, Hussen Bashe.

Amesema, Wananchi kutoka mikoa ya jirani na mikoa yote ya Tanzania wanatakiwa kushiriki katika maadhimisho hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Stendi ya zamani ya Wilayani Babati Mkoani Manyara.

Kwa upande wao baadhi ya Wwananchi wanaeleza umuhimu wa maadhimisho hayo kwani yataongeza Kilimo chenye tija kwa jamii.

Kikoti: Jamii iachane na matumizi holela ya Dawa
Maisha: Fanya hivi upate Kazi au Ajira kirahisi