Maafisa elimu wa Halmashari, wametakiwa kuacha tabia ya kuzalisha madeni kwenye Halmashauri zao kwa watumishi wa sekta ya elimu jambo ambalo hupelekea Serikali kupata hasara.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajjat Fatma Mwasa katika uzinduzi wa Semina ya Chama cha Walimu Tanzania ya ujirani mwema wa kanda ya ziwa na kanda magharibi mwaka 2024.
Semina hiyo, ilishirikisha mikoa nane iliyojumuisha washiriki 450 kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt, Doto Biteko ndani ya Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera ikilenga kuwakutanisha Viongozi hao na kutatua changamoto zao.
Amesema, “ukiangalia Orodha ya madeni zinatofautiana sana Halmashari moja na nyingine unapokutana na afisa elimu anayejali anaepuka sana madeni pale unapokuta afisa elimu asiyejali hatiliii uzito utakuta lundo la madeni mara walimu wemeenda likizo wengine wanahamishwa, Walimu mtusaide kuwahimiza.
Awali, akisoma taarifa ya Chama hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CWT, Katibu wa Chama cha Walimu Mkoa wa Kagera, Njile Lufasinza amesema kwa sasa bado wanakabiliwa na changamoto ya kikokotoo, madeni ya walimu kutolipwa kwa wakati, hasa Mkoa wa Kagera ambao Walimu wanadai bilioni mbili.