Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha Mkoani Pwani, imeingia makubaliano kwa mara ya pili ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Renmin cha Nchini China, katika nyanja za mbalimbali zikiwemo za mafunzo, utafiti na kubadilishana wataalamu.

Wakisaini hati hizo, Mkuu wa Shule ya Mwalimu Nyerere Prof. Marcellina Chijoriga na Kiongozi Mkuu wa Chama Tawala cha China – CPC, Zhang Donggang wamesema Wataalamu watakuwa wakienda China na Tanzania, ili kubadilishana uzoefu huku akibainisha kuwa chuo cha Renmin kinauwezo wa kuwajengea uwezo viongozi wa chama na Serikali.

Amesema, “Chuo hicho ni kikubwa sana na cha muda mrefu na kiko vizuri kwenye masuala ya utafiti wa uandishi wa vitabu na katika masuala ya uandishi wa vitabu ambapo ushirikiano huo utakuwa na manufaa makubwa sana kwa pande zote mbili. Faida ni kwa vyama sita vya ukombozi Kusini mwa Afrika, China wamesaidia ujenzi wa shule hiyo ambavyo ni CCM, FRELIMO, SWAPO, ANC na ZANU-PF msaada kutoka chama cha ukomunisti cha nchini China CPC.”

Prof. Chijoriga alisema chuo hicho kilichopo Beijeng kilianza ushirikiano mwaka jana ambapo uongozi wa Shule walikwenda na katibu mkuu wa CCM wakati ule Chongolo na sasa imeanza safari mpya kwa kusaini mikataba hiyo kwani kina uzoefu mkubwa nani cha zamani sana.

Naye Naibu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Dkt. Evaristo Haule alisema China imefanikiwa na wameona namna gani kutumia njia ili kuona wao wamefanyaje na kufikia hatua kubwa kiasi hicho kwenye maendeleo na CPC inavyotoa dira kuongoza nchi yao.

Naye Dk Theresia Dominick kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam akizungumza kwa niaba ya Wakufunzi Mkufunzi wa Shule ya Mwalimu Julius Nyerere amesema kuwa kupitia wenzetu wachina tujifunze kuwa na nidhamu ya kufanya kazi kwa bidii.

Kwa upande wake Kiongozi huyo kutoka China, Zhang Donggang alisema ushirikiano uliopo baina ya China na Tanzania na nchi nyingine ni katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo ambapo wao wanaangalia sana maslahi ya wananchi na kwambawanapaswa kushikana mkono katika kuhakikisha zinapiga hatua kwenye masuala ya kimaendeleo, ili kudumisha umoja uliopo.

Maisha: Waleta dharau eti nao wanashangaa kudharauliwa
Uchaguzi Serikali za Mitaa: Toima awapa neno Wananchi Manyara