Benki Kuu ya Tanzania pamoja na Bodi ya Bima ya Amana (DIB) inashiriki maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani yanayofanyika katika viwanja vya Chamanangwe kisiwani Pemba.
Maonesho hayo yamezinduliwa rasmi Oktoba 10, 2024 na mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla.
Maonesho hayo yameanza Oktoba 7, 2024 yanatarijwa kumalizika Oktoba 20, 2024 yakiwa na kauli mbiu isemayo, “Haki ya Chakula kwa maisha bora ya sasa na baadae.”
Mgeni Rasmi katika maonesho hayo ni Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla ambaye wakati wa ufunguzi alibainisha kwamba kwenye maadhimisho hayo watu watajionea na kujifunza kuhusu vyakula vya asili.
Vyakula hivyo ni vile vinavyopatikana kwenye visiwa vya Pemba na Unguja sambamba na kutoa elimu ya lishe, ili kupunguza tatizo la udumavu kwenye jamii.
Wakati huo huo, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shamata Shaame Khamis ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania pamoja na Bodi ya Bima ya Amana kwa kushiriki Maonesho hayo ya siku ya chakula Duniani.
Maonesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya Chamanangwe Kisiwani Pemba yanalenga kuwasaidia wanacnhi kutambua alama muhimu zilizopo kwenye noti, majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania pamoja na majukumu ya Bodi ya Bima ya Amana.
Waziri Shamata, alitoa pongezi hizo Oktoba 10, 2024 alipotembelea banda la BOT na DIB.