Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 14, 2024 ameshiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbulizi ya Hayati Julius Kambarage Nyerere, iliyofanyika katika Kanisa la Mt. Francis Xavier Nyakahoja, Jijini Mwanza.

Ibada hiyo, imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwemo Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko.

Jinsi Kamanda wa Jeshi alivyompa maswali Baba wa Taifa
Tofauti yetu ni uwezo wa kuamua baada ya kufikiri - Mwl. Nyerere