Kurejea kwa Aishi Manura na Ayoub Lakred kunaifanya Simba kuwa na jumla ya magolikipa 6 kuelekea Dabi ya Kariakoo.

Golikipa Ayoub Lakred amerejea mazoezini na wachezaji wenzake kwa mara ya kwanza tangu alipopata majeraha mwezi Agosti,Ayoub yuko fiti kwa 100% na anashiriki kikamilifu mazoezini.

Uwepo wa Moussa CamaraA,youb,Allg Salim,Aishi Manula,Hussein Abel na Feruzi Teru unampa wakati mgumu kocha Fadlu Davies kuchagua golikipa wa kumuanzisha katika mechi hiyo.

Mashabiki wa Simba wanaamini kocha Fadlu atampa kipaumbele moussa Camara kutokana na ubora aliouonyesha kwenye michezo mbalimbali hivi karibuni.

Baadhi ya mashabiki wa Simba wamenukuliwa wakisema

“Huu ni mchezo muhimu uliobeba hisia za Watanzania na kocha anapaswa kuwa makini Sana katika uchaguzi wake wa kikosi cha kwanza.Mashabiki hawataki kupoteza mchezo huo kwa namna yoyote,kocha awapange wachezaji anaowajua kwa ubora wao na si shinikizo kutoka kwa watu wengine ”

Simba wanapaswa kushinda mchezo huo muhimu ili kujiimarisha kuelekea mbio za ubingwa wa ligi kuu NBC.

Wajadili mpango kazi utekelezaji hoja za Wauguzi
Simba hawana cha kupoteza Kariakoo Dabi