Na Humphrey Edward.

Miaka 22,000 iliyopita, kulikuwa na kundi kubwa zaidi la Wanadamu duniani, wakifahamika kama Wakhoisan, kabila la wawindaji-wakusanyaji lililopatikana kusini mwa Afrika.

Leo, ni Wakhoisan 100,000 tu, ambao pia wanajulikana kama Bushmen, wamesalia, ambapo Profesa katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Nanyang huko Singapore, Stephan C. Schuster alichapisha utafiti mpya kuhusu kabila hilo, unaeleza kuwa wengi wao sasa wanaishi katika umasikini,  na kudai kuwa mila zao za kitamaduni ziko hatarini kutoweka.

Nini kilitokea.

Alisema, watu bilioni 7 sasa wanaoishi duniani hufanya iwe vigumu kwao kuelewa jinsi watu wachache walivyoishi zamani maana karibu miaka 10,000 iliyopita, hakukuwa na zaidi ya Watu milioni 1 kwenye sayari.

Wawindaji-wakusanyaji ambao bado wanaishi kwa kutegemea uwindaji Nchini Namibia. Utafiti mpya wa kijeni unaonyesha walikuwa kundi kubwa zaidi la wanadamu hapo awali. Picha ya Stephan C. Schuster/Chuo Kikuu cha Jimbo la Penn.

Na miaka 100,000 iliyopita, watu 10,000 ni wachache na kwamba mfuatano mzima wa jenomu uliochanganuliwa unaonesha kwamba kuna wakati watu wasiokuwa Wakhoisan walikuwa hawafanyi vizuri kama Wakhoisan.

Mabadiliko ya hali ya hewa, kabla ya miaka 22,000 iliyopita, sehemu ya kusini mwa Afrika ambako Wakhoisan waliishi ilikuwa na mvua nyingi zaidi, ikilinganishwa na sehemu kavu za magharibi na kati ya bara ambako vikundi vingine viliishi.

Hali ya hewa kavu ilimaanisha uwepo wa Wanyama pori wachache na chakula kidogo, ambayo inatafsiriwa kuwa wakati huo wangezaliwa watoto wachache.

Kwa hivyo idadi nyingine ilipungua kwa kiasi kikubwa wakati idadi ya Wakhosian ilibaki sawa, lakini baada ya enzi ya mwisho ya barafu kuisha, hali ya hewa ilibadilika na kwa sababu ambazo hazikueleweka idadi ya watu wengine wa Afrika iliongezeka, na ukuaji mkubwa wa Wanadamu duniani kote ulianza.

Athari.

Tunaona mwisho wa utamaduni wao na mtindo wao wa maisha wa uwindaji, ambao unabadilishwa na mazingira ya ufugaji na kilimo, kwa mfano Nchini Botswana, kuna sheria kwamba wawindaji hawawezi kuruhusiwa kuwinda tena.

Kuna migogoro ya ardhi na mara nyingi wanaondolewa kutoka katika ardhi waliyokuwa wakiwinda au kuiona kuwa takatifu kulingana na tamaduni zao, wakichukuliwa kama watu wa hali ya chini katika jamii na wana uwakilishi mdogo sana wa kisiasa.

Chifu Ouma Katrina Esau mwenye umri wa miaka 88 (kwa mwaka 2017), anaaminika kuwa ndiye Mwafrika Kusini wa mwisho aliyesalia, anayeweza kuzungumza lugha ya kale ya Kikhoisan San, N|uu. Lugha hii ina umri wa miaka 25,000 na alichapisha kitabu katika N|uu kilichoitwa Skilpad en Volstruis Tortoise and Ostrich Mei 2021.

Khoisan ni nini.

Hili ni neno linalowakilisha Watu, ambalo linaloweza kufahamika kwa watu wa kiasili wa Kusini mwa Afrika ambao kimapokeo huzungumza lugha zisizo za Kibantu, wakichanganya watu wa Khoekhoen na Wasan.

Khoisan, pia wanajulikana kama Khoi-San, ni kabila linalopatikana kusini mwa Afrika, hasa katika eneo linalozunguka Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Angola na Zimbabwe.

Muda mrefu kabla ya kuwasili kwa Wabantu, Khoisan wanachukuliwa kuwa wakazi wa kwanza wa nchi hizi. Wanachukuliwa kuwa moja ya makabila ya zamani zaidi katika eneo hilo, yenye historia na utamaduni unaochukua maelfu ya miaka.

Neno “Khoisan” ni neno linalotumiwa kurejelea vikundi viwili tofauti vya lugha na vinasaba, ambayo kiutamaduni ni kawaida kwani kila kabila huwa na taratibu zake za kimaisha na namna ya kuelewana ili kuweza kuendesha maisha yao ya kila siku.

KHOI.

Watu wa Khoi, pia wanajulikana kama Khoikhoi au Khoekhoe, ni Wafugaji wa kijadi na siku zote wamekuwa wakichunga Ng’ombe kama mojawapo ya vyanzo vyao vikuu vya kuendesha maisha.

Wanajulikana pia kwa lugha zao za kikonsonanti za kubofya, ambazo zina sauti za kipekee za kubofya kama sehemu ya hotuba yao na walitawanyika kihistoria katika maeneo ya magharibi na kusini mwa Afrika Kusini.

SAN.

Watu wa San, pia wanajulikana kama Bushmen, ni Wawindaji wanaojulikana kwa ujuzi wao wa kina wa kimazingira na mbinu za jadi za uwindaji, wakiwa na anuwai ya lugha, nyingi ambazo pia zina sauti za kubofya.

Kihistoria, Watu wa San waliishi eneo kubwa zaidi kusini mwa Afrika, pamoja na Jangwa la Kalahari na ieleweke kwamba anatomia kimwili hawa Wakhoisan kwa wastani ni wafupi na wembamba zaidi kuliko watu wengine wa Kiafrika.

Kwa kuongezea, pia wana rangi ya ngozi ya manjano na mikunjo ya epicanthal machoni pao, mithili ya Wachina na watu wengine wa Mashariki ya mbali.

Baadhi ya sifa hizi sasa zimekuwa ni za kawaida kwa makabila mengine ya Afrika Kusini, mfano wa muonekano wa kabila la Nelson Mandela.

Sifa nyingine ya kimaumbile ya Khoisan ni steatopygia ya Wanawake (maendeleo makubwa ya baadaye ya ukuaji wa makalio), ambayo yalisababisha mwanamke mmoja kupelekwa Ulaya katika karne ya 19 na kutumika kuoneshwa kwenye maonesho, maarufu Venus Hotten (hili tutalizungumza siku nyingine).

Somo.

Sababu muhimu zaidi ya mabadiliko katika idadi ya watu ni hali ya hewa ni jambo la msingi watu wanatakiwa kulifahamu kwamba kuna wakati kulikuwa na wanadamu wachache, waliolikaribia kupotea kulingana na uhalisia wa maisha kimazingira.

Huu pia ndio muundo tunaouona katika spishi zilizo hatarini kutoweka hii leo. Tunajiona kuwa hatuwezi kuathiriwa, lakini hatupaswi kuchukua kuwa hali ya hewa haitabadilika katika siku zijazo kwa njia ambazo zitatuhatarisha.

Kiufupi, tunahitaji kufahamu kwamba hali ya hewa tuiangalie kwa uzito wa kipekee na kuendana na mazingira halisia ili kujiokoa ama kuandaa mazingira ya wakati ujao ili historia isipotee ama itunzwe vizuri kwa matumizi ya vizazi vijavyo.

Kenya: Kindiki apendekezwa kurithi mikoba ya Gachagua
Wajadili mpango kazi utekelezaji hoja za Wauguzi