Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TanTrade, Latifa Khamis, akiwasilisha faida za kibiashara zilizo patikana katika siku ya hitimisho ya Kongamano na Uchumi na Biashara baina ya Tanzania na Iran.
Kongamano ilo la Uchumi na Biashara limedumu kwa takribani siku nne, likikutanisha wadau wa biashara kama vile, kilimo, madawa, madini, viwanda, uvuvi, kahawa, mafuta, gesi, nk, kutoka nchi zote mbili yaani Tanzania na Iran.
Biashara kubwa zimefanyika, michakato ya uwekezajı imeanza hususani kwa Tanzania, kongamano ilo limeratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), leo katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere, Dar es Salaam Tanzania.