Liverpool wameendelea kufanya vyema ligi kuu Uingereza baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya chelsea. Penati ya Mohammed Salah dakika ya 29 ilifungua milango ya mabao kwa Liverpool na lilidumu kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza. Dakika ya 48 Chelsea walisawazisha bao hilo kupitia kwa Nicolas Jackson lakini Curtis Jones aliipa Liverpool bao la pili akimalizia pasi ya Mohammed Salah dakika ya 51.

Matokeo hayo yanaifanya Liverpool kufikisha alama 21 wakiongoza msimamo wa ligi kuu Uingereza katika mechi 8 walizocheza, Chelsea wanasalia katika nafasi ya 6 wakiwa na alama 14.

Manchester City wameendelea kufanya vizuri baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Wolves . mabao ya  Gvardiol na John Stones yaliifanya City kufikisha alama 20 katika michezo 8 waliyocheza. Ushindani wa ubingwa umeendelea kuwa mkali kwa Liverpool ,Manchester City ,Arsenal na Aston villa baada ya timu hizo kucheza michezo nane na kusalia nafasi 4 za juu.

Manchester United imeanza kurejesha  matumaini kwa mashabiki wake baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Brentford. Mabao ya United yaliwekwa kimiani na Garnacho dakika ya 47 pamoja na Hojlund dakika ya 62.Matokeo hayo yameifanya United kupata ushindi wa tatu wa EPL katika mechi 8 wakipoteza mechi 2 na sare 3 hivyo kujikusanyia alama 11 pekee wakifunga maba0 7 na kufungwa 9 wakishika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi.

Yanga yatuma salamu jeshini baada ya kuisambaratisha Simba
Barca yarejea kileleni kwa kishindo