Klabu ya Yanga imeendelea kufanya vyema ligi kuu ya NBC baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani wao wa jadi Simba. Ushindi huo umeifanya Yanga kujikusanyia alama 15 katika michezo 5 iliyocheza mpaka sasa wakishika nafasi ya 2 nyuma ya Singida Black Stars yenye alama 19 wakicheza michezo 7.

Msimu huu Yanga imeuanza vyema baada ya kufunga mabao 9 katika mechi 5 na haijaruhusu bao lolote. Timu hiyo chini ya kocha Gamondi itapanda tena dimbani hapo kesho kuvaana na JKT Tanzania mchezo utakaopigwa dimba la Azam Complex.Mchezo huo ni muhimu kwa Yanga kuelekea kileleni na kama wataibuka na ushindi basi watafikisha alama 18 wakiwa na mchezo mmoja. Mchezo huo unategemewa kuvutia watazamaji wengi kutokana na ubora waliounyesha mpaka sasa .

JKT wanapaswa kushinda mchezo huo baada ya kujikusanyia alama 10 katika mechi 7 na wanashikilia nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi hivyo kama watashinda mchezo huo basi watapanda mpaka nafasi ya 5 wakiwa sawa kwa alama na Simba,Fountain Gates wenye alama 13.

 

Fadlua azitaka alama tatu za Tanzania Prisons
Liverpool,Man City na united zaing'arisha wikiendi