Klabu ya Simba imewasili jijini mbeya kukabiliana na Tanzania prisons  mchezo wa ligi kuu ya NBC.Simba imewasili mbeya ikiwa na maumivu ya kupoteza alama 5 katika michezo miwili iliyocheza hivi karibuni. Simba ilipoteza alama mbili katika mchezo dhidi ya Coastal Union mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 mchezo ambao Simba walikuwa mbele kwa mabao 2 kipindi cha kwanza lakini Coastal walisawazisha mabao hayo.

Mchezo wa pili walipoteza alama zote tatu kwa kukubali kufungwa  bao 1-0 na watani zao wa jadi Yanga . Huu ni mwanzo mbaya kwa Simba msimu huu baada ya kupoteza alama 5 katika michezo 6 . kwa sasa timu hiyo ina alama 13 ikishika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi huku Singida Big Stars anaongoza ligi akiwa na alama 19 katika michezo 7 .

Kwa upande wa Tanzania Prisons wao wamecheza michezo 7 na wamejikusanyia alama 7 wakishika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC. Mchezo wa Simba na Tanzania Prisons utapigwa siku ya jumanne saa 10:oo jioni dimba la Sokoine Mbeya

Simba wanapaswa kushinda mchezo huo na kocha huyo amefunguka kwa kusema

‘Tunawaheshimu prisons wana timu nzuri .Matokeo yanaonyesha sio rahisi kuwafunga hasa wakiwa nyumbani lakini tumekuja hapa tukiwa na kazi ya kufanya na kazi yenyewe ni kuchukua alama tatu.Ni mechi ambayo tunatakiwa kushinda”

Naye nahodha msaidizi Mohammed Hussein amenukuliwa akisema

”Kesho tutakuwa na mchezo mgumu dhidi ya Prisons na hasa tukiwa hapa mbeya ,Tumejiandaa vizuri kwenda kufanya vizuri.Tumekuja Mbeya kupata alama tatu”

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 22, 2024
Yanga yatuma salamu jeshini baada ya kuisambaratisha Simba