Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, Faiza Salim amewataka Wananchi Wilayani humo kutumia Nishati Safi ya Kupikia na kuacha kutumia Kuni Na Mkaa, ili kuepuka tabia ya ukataji wa Miti, jambo ambalo linaweza kusababisha ukosefu wa Mvua za mara kwa mara.

Akiwahamasisha Wananchi wa Wilaya ya Busega Mkoani humo, Faidha amesema Wamama wengi wa Wilaya hiyo wamekuwa wakitumia Kuni na Mkaa Jambo ambalo linaweza kuwasababishia magonjwa ya Moyo na Mapafu na kuwataka waanze kutumia Nishati Safi ya Kupikia.

Amesema, “kwa wakati tuliofikia tunatakiwa kuacha kutumia Kuni na Mkaa na Wamama wengi na jamii ya Busega wanatumia kuni na kukata sana Miti tunajua athari za ukataji wa Miti tumekuwa tukikata sana Miti kwa ajili ya kutafuta Kuni na tumeona mabadiliko ya Tabia Nchi yanavyoathiri Kilimo na mambo mengi ya kimazingira, hatupati Mvua kwasababu ya ukataji wa Miti.”

Tanzania, Singapore kuimarisha uhusiano, Biashara
Tanzania yasaini Hati ya ushirikiano uwekezaji, mafunzo