Johansen Buberwa – Kagera.
Watanzania wameaswa kulinda vyanzo vya maji pamoja na kutunza Mazingira ikiwemo kuacha tabia ya kukata Miti hovyo ili kusaidia kutunza vyanzo hivyo na taifa kubaki hewa safi.
Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya semina iliyofanyika manispaa ya Bukoba Mkoani humo, Afisa Mradi shirika la Kwawaze, Ackilinah Mbyellah amesema mradi huo ni wa majaribio na wana mpango wa kuzifikia Wilaya tano za mkoa huo kwa watu zaidi 138,000.
Mbyellah amesema kama Shirika la kwa wazee wamakuja na mpango wa kuielimisha jamii ili kuepusha ihalibifu wa mazingira kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa wale wanao kata miti hovyo na kutupa taka wengine wanalima karibu na vyanzo vya maji tunatamani jamii nzima iweze kufahamu kwa kwa kupata elimu ili kusaidia vizazi vijavyo.
“Watafiti wanasema kufikia mwaka 2050 ukihesabu mtu mmoja hadi sita lazima kutakuwa na wazee hapo katikati kama hatujavilinda vyanzo vya maji vinaweza kuwa vimekauka” amesem Afisa Mradi shirika Mbyellah.
Naye Afisa Mazingira Mkoa Kagera Primtiva Pastory amesema mkoa huo ni miongoni mwa mkoa inayokabiliwa na changamoto ya tabia ya nchi ikiwemo mvua kuchelewa kunyesha kwa wakati ikulinganishwa na misimu iliyopita ambapo mvua za vuli zilikuwa zinaanza Julai na Agosti.
Amesema, “na kwa sasa inaanza mwezi wa kumi na kutumia furusa hiyo kuwahimiza wanachi kuendelea kufatilia vyombo mbalimbali vya habari ili kuwasikiliza wataalamu wanavyo washauri namna ya kulinda na kutunza mazingira.”