Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe ameagiza Mamlaka za Udhibiti na Usimamizi wa Biashara Nchini kuachana na dhana ya kukimbilia kufunga na kukwamisha Wajasiriamali wadogo ambao hawajatimiza vigezo vya kisheria badala yake wawe walezi kwa kuwaelekeza hatua za kufuata, ili wawe walipa kodi wakubwa.
Kigahe ametoa Maelekezo hayo wakati akifungua maonesho ya tatu ya Biashara ya Tanzanite Manyara Trade Fair 2024 Mjini Babati, yaliyohudhuriwa na Wajasiriamali kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji Chama cha Wafanyabiashara – TCCIA Mkoa wa Manyara, Zainabu Rajabu amesema maonesho ya mwaka huu yamehudhuriwa na washiriki 337.
Maonesho hayo, yamefanyika chini ya kauli mbiu ya “Manyara kwa ustawi wa biashara na uwekezaji” huku baadhi ya wajasiriamali walioshiriki wakifurahia kukutanishwa na wateja ma marafiki wa kibiashara.
Maonesho ya tatu ya Biashara ya Tanzanite Manyara trade fair 2024 yaliyoanza Oktoba 20 yataendelea hadi Oktoba 30.