Klabu ya Namungo imemkaribisha rasmi Juma Mgunda kuwa kocha mkuu wa timu hiyo baada ya kumbadilishia majukumu Mwinyi Zahera. Mgunda anachukua mikoba ya Zahera aliyefanya vibaya kwa kucheza michezo 7 ya ligi ya NBC akivuna alama 6 na kushika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi.

Mgunda atashirikiana na makocha wasaidizi ambao ni  Ngawina Ngawina ,Shadrack Nsajigwa na Vladimir Niyonkuruhuku na Mwinyi Zahera akiwa ni moja ya washauri wanaounda benchi la Ufundi. Mgunda amekabidhiwa timu hiyo kuelekea mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Simba .Mchezo huo utakaopigwa oktoba 25 dimba la KMC jijini Dar es salaam hivyo ana siku moja tu kujiandaa na waajiri wake wa zamani.

Mpaka sasa Namungo wameshinda mechi mbili na kupoteza mechi tano. Kama wataibuka  na ushindi dhidi ya Simba watafikisha alama 9 na kupanda mpaka nafasi ya 10 wakilingana kwa alama na Dodoma Jiji. Kwa upande wa Simba wao wana alama 16 kama watashinda mchezo huo basi watafikisha alama 19 sawa na Singida Black Stars na kukaa kileleni kwa uwingi wa mabao ya kufunga.

Juma Mgunda na Historia ya Simba 

Msimu wa 2022/23 Juma Mgunda aliuanza kama kocha mkuu wa Coastal Union lakini baadaye alitua Simba kama kocha mkuu wa muda  akichukua nafasi ya Franco Martinez aliyeshindwa kufikia vigezo vya kuwa na leseni ya CAF daraja A kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Africa.Mgunda aliisaidia Simba kumaliza nafasi ya pili ligi kuu na kufika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Africa.

Msimu wa 2023/24 Kocha huyo alibadilishiwa majukumu kwa kukabidhiwa  Simba Queens na aliisaidia timu hiyo kutwaa kombe la ligi kuu ya wanawake (TWPL) NA kufika nusu fainali kufuzu ligi ya mabingwa Africa ukanda wa CECAFA. Licha ya mafanikio hayo makubwa kocha huyo aliachana na Simba mwanzoni mwa msimu wa 2024/25 na sababu kubwa ikitajwa ni maslahi ya pande zote mbili.

 

 

Nishati Jadidifu: Serikali kuendelea kuwashirikisha Wawekezaji
Dkt. Rubai apandishwa kizimbani kwa ubakaji