Manchester City wanavutiwa na mshambuliaji wa Uswidi Viktor Gyokeres, Xavi anataka kumchukua Raphinha kutoka Barcelona ikiwa atakuwa kocha wa Manchester United na Antony anawaniwa na Uholanzi.
Manchester City wanatazamia kumnunua mshambuliaji wa Sporting na Uswidi Viktor Gyokeres, 26, kama mbadala wa muda mrefu wa Erling Haaland. (Sky Sport Switzerland, via Mirror)
Kocha wa zamani wa Barcelona Xavi anataka kumleta Trafford winga wa Brazil Raphinha mwenye umri wa miaka 27 ikiwa atachukua nafasi ya Erik ten Hag kama mkufunzi wa Manchester United. (Fichajes – kwa Kihispania)
Winga wa Manchester United Mbrazil Antony, 27, anaweza kupewa fursa ya kutoka Old Trafford na klabu yake ya zamani Ajax, lakini wababe hao wa Uholanzi wanasemekana hawajaridhishwa na mpango huo. (De Telegraaf, kupitia Mirror)
Aston Villa wako tayari kumpa mlinda lango wa Poland Oliwier Zych mwenye umri wa miaka 20 kandarasi mpya huku Arsenal na Brighton wakiripotiwa kumtaka. (Football Insider)
Barcelona wanamfuatilia mshambuliaji wa River Plate raia wa Argentina, Felipe Esquivel, 16. (Sport – kwa Kihispania)
Real Madrid wanapanga kumpa beki wa Liverpool na England Trent Alexander-Arnold, 26, kandarasi ya kati ya euro milioni 14-15 kwa mwaka hadi msimu wa 2029-30. (Caught Offside)
Pep Guardiola ameiomba Manchester City kumfuatilia beki wa RB Leipzig Castello Lukeba, 21, huku mkufunzi huyo wa Manchester City akitamani kumnunua Mfaransa huyo msimu ujao. (Fichajes – kwa Kihispania)
Barcelona na Arsenal wanavutiwa sana na mshambuliaji wa Colombia na Aston Villa Jhon Duran, 20, na The Gunners wanaweza kuwa katika nafasi nzuri zaidi kumsajili. (Fichajes – kwa Kihispania)