Serikali Nchini, imesema inaandaa mpango wa kwa kila Halmashauri nchini kuwa na misitu ya asili ili kuimarisha mkakati wa usimamizi wa biashara ya kaboni na uhifadhi wa mazingira.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Ashatu Kijaji wakati wa ziara yake Mkoani mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua, kufungua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo.

Amesema, lengo la Serikali ni kuhakikisha kila halmashauri nchini inaingia katika biashara ya kaboni kupitia upandaji wa miti ambapo pamoja na uhifadhi wa mazingira, miti pia ni fursa ya kibiashara inayowezesha jamii kujiongezea kipato kwa wananchi na jamii kwa ujumla.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza jambo wakati wa kuzindua Shule ya Sekondari Kiomoni iliyopo Kata ya Mzizima Halmashaurii ya Jiji la Tanga mkoani Tanga. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Japhari Kubecha.

Dkt. Kijaji ameongeza kuwa, mpango huo mbali na ushirikishaji wa Halmashauri pia utawalenga wananchi wanaomiliki maeneo makubwa ya ardhi wenye uwezo wa kutumia maeneo yenye ukubwa wa ekari tano hadi 10 kwa ajili ya kupanda miti kibiashara.

“Pamoja na fursa ya biashara, kupitia upandaji miti kutasaidia kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi ambapo yanasababisha mabadiliko ya hali ya hewa ikiwemo ongezeko la joto na mvua zisizo na mpangilio,” amesema Dkt. Kijaji.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) akitazama samani mbalimbali zilizopo katika jengo la maabara katika Shule ya Shule ya Sekondari Kiomoni iliyopo Kata ya Mzizima Halmashaurii ya Jiji la Tanga mkoani Tanga. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Japhari Kubecha na kulia kwa Waziri Kijaji ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batlida Burian.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian amesema Ofisi yake imekuwa ikiendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu athari za uharibifu wa mazingira ikiwemo uchomaji ovyo wa misitu na kuwahimiza kupanda miti kwa ajili ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira.

Ameongeza Mkoa huo una zaidi ya hekta 700,000 za misitu zenye mashamba matatu ya miti, ambapo katika kuendelea kutunza maeneo hayo ofisi yake kwa kushirikiana na mamlaka na idara mbalimbali za serikali imekuwa ikiwahimiza wananchi kutunza maeneo hayo na kuacha kuuingiza mifugo ndani ya hifadhi hizo.

Amefafanua kuwa Wananchi wamekuwa na mwamko mkubwa katika kilimo cha mikoko ambacho kinasaidia katika utunzaji wa mazingira ya bahari kwani wakati wa mmomonyoko wa udongo miti hiyo inasaidia kusitokee uharibifu wa mazingira.

Dkt. Kijaji yupo katika ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Tanga iliyoanza Oktoba 23, 2024 kwa ajili ya kukagua kwa ajili ya kukagua, kufungua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo.

Pangani: Wapatiwa fedha kunusuru viumbe Bahari
Mchengerwa: Vyama vihamasishe Wanachama wao kugombea