Mkutano wa pili wa BRELA na Wadau wake umeganyika hii leo Oktoba 25, 2024 uliolenga kujadili mafanikio, fursa na changamoto mbalimbali na kuona namna ya kuzitatua, ili kuboresha huduma katika sekta ya Viwanda na Biashara

Ufunguzi wa mkutano huo, umefanyika jijiji Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwani  Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe.

Amesema, mkutano huo unaunga mkono juhudi za Serikali za kuweka mazingira wezeshi kibiashara, ili yaendelee kuwa bora hadi ifikapo 2025, pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya sekta za umma na binafsi.

Kigahe ameongeza kuwa, pia mkutano huo unatoa nafasi kwao kujipima na kujitathimini katika kutoa huduma na kuziboresha katika mfumo wa kusomana wa TNBP.

Miongoni mwa Taasisi za serikali zilizotajwa kufanya kazi na BRELA katika mfumo huo ni pamoja na NIDA, TRA, TCRA na CEPG lengo likiwa ni kuwezesha upatikanaji wa Leseni za biashara kundi “A” kuwa wa rahisi na haraka.

Wadau wengine walihudhuria Mkutano huo ni Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya Brela Prof. Neema Mori, Afisa Mtendaji Mkuu BRELA, Godfrey Nyaisa.

Wengine ni Watendaji kutoka ofisi ya katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na wadau wengine kutoka katika sekta hiyo.

Kauli mbiu katika mkutano huo ni ” Mifumo ya Kitaasisi inayosomana na uwezeshaji wa biashara nchini.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 26, 2024
Maisha: Ataja mbinu kumrejesha Mume aliyetoa talaka