Ni tukio la utambuzi wa majukumu ya kijamii, ambalo leo linadhihirishwa na baadhi ya wafanyabiashara wa Soko la Machinga Complex lililopo jijini Dodoma.
Kwa pamoja wamejumuika kutoa msaada kwa Watoto yatima waliopo katika kituo cha Ndachi wakiongozwa na Katibu wao Marco Simon huku wakisema dhamira yao ni kushirikiana na jamii lakini pia kuwasaidia wahitaji.
Hata hivyo wamenang’amua sababu zilizowasukuma kutoa msaada huo wakisema Watoto hao wanahitaji faraja, msaada wa kiuchumi na kiroho.
Wafanyabiashara hao hawakuishia tu kutoa msaada, waliwaasa Watoto hao kutokujihisi wapweke na kwamba wanatakiwa kutambua kuwa wapo watu wanaowajali na wanaweza kuwa msaada katika safari yao ya maisha.
Mbali na kwamba hii ilikuwa ni fursa nzuri ya kuwapa matumaini, lakini pia Mlezi wa watoto katika kituo hicho, Said Kulele alitoa shukrani zake kwa Wafanyabiashara akisema msaada huo ni muhimu na mahitaji yao ya kila siku.
Aidha, aliwasisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kijamii katika kusaidia watoto yatima huku akiwahamasisha wengine kuiga mfano wa Wafanyabiashara hao wa Machinga Complex.
Tukio hili limeoesha nguvu ya mshikamano katika jamii na umuhimu wa kusaidiana kama sehemu muhimu ambayo inachangia kuboresha maisha ya Watoto yatima