Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Musuguri amefariki dunia hii leo Oktoba 29, katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza 2024 alipokuwa akipatiwa matibabu.
Jenerali Musuguri alikuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kati ya mwaka 1980 hadi 1988 wakati wa Serikali ya Awamu ya kwanza chini ya Hayati Mwl. Julius Nyerere na amefariki akiwa na miaka 104.
Aliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania – JWTZ, kuukomboa Mkoa wa Kagera wakati vita dhidi ya Uganda iliyokuwa chini ya Iddi Amin baada ya uvamizi wa Novemba 1978 Mkoani Kagera.
Brigedia Jenerali David Musuguri alizaliwa January 4 mwaka 1920 Butiama Mkoani Mara na aliitumikia Nchi kuanzia Mwaka 1942 hadi 1988, akihitimisha Uongozi wake kama Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kati ya 1980 na 1988.
Alianza kazi yake kijeshi katika King’s African Rifles (KR) na Tanganyika Rifles kabla ya kujiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na alishiriki pia vita Kuu ya Pili ya Dunia, Battle of Simba Hills nq Battle of Madagascar.