Idadi ya watu waliofariki kwaa mafuriko nchini Hispania imefikia watu 95, baada ya maeneo mengi kufunikwa kwa Maji huku Watu 92 kati ya hao wakifariki katika mji wa Valencia pekee.
Kupitia taarifa iliyochapishwa katika mtandao wa X na Kitengo cha Huduma za Dharura Nchini humo, imeelezwa idadi ya watu ambayo bado haijafahamika hawajulikani walipo, huku maeneo kadhaa yakiwa hayawezi kufikiwa kutokana na mafuriko hayo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, miili mingine miwili imepatikana katika eneo jirani la Castilla-La Mancha, huku mtu mmoja akifariki katika mji wa kusini wa Malaga.
Kufuatia tukio hilo, lililosababisha sehemu kubwa mji wa Valencia kutofikiwa sasa usaidizi unafanywa kwa kutumia helikopta na watu wengi wakiwa wakiomba usaidizi kupitia mitandao ya kijamii.