Kufuatia Mahakama Kuu Nchini Kenya kuondoa amri iliyokuwa imewekwa ya kuzuia kuapishwa kwa Prof. Kithure Kindiki kama Naibu rais wa Kenya, Mkuu wa Watumishi wa umma, Felix Kosgei ameunda kamati ya watu 23 itakayokuwa na jukumu la kutayarisha sherehe ya kuapishwa Kiongozi huyo.

Mapema hapo jana Oktoba 31, 2024, Jopo la majaji watatu Eric Ogola, Anthony Mrima na Fredah Mugambi, walisema amri iliyokuwa imetolewa na Mahakama Kuu ya Kerugoya imeondolewa lakini wakasema waliofungua kesi wana haki ya kukata rufaa.

David Munyi Mathenge na Peter Gichobi Kamotho walikuwa wameomba mahakama kuzuia kuapishwa kwa Kindiki baada ya Bunge kuidhinisha uteuzi wa Kindiki kuwa Naibu rais baada ya Bunge la Senate kumuondoa ofisini Righathi Gachagua.

Hata hivyo, Majaji wamesema kesi ya Gachagua kupinga kuondolewa ofisini itasikilizwa kuanzia siku ya Alhamisi Novemba 7, 2024 na kwamba Gachagua ana haki ya kukata rufaa kuhusiana na hatua iliyoamriwa.

Serikali kuendeleza ukarabati wa Shule Kongwe - Katimba
Israel: Shambulizi la anga la Hezbollah lauwa saba Shambani