Mauaji ya Waandishi wa Habari kote duniani yaliongezeka katika mwaka wa 2022 na 2023 ikilinganishwa na miaka miwili kabla ya kipindi hicho.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika moja la Umoja wa Mataifa la Utamaduni – UNESCO, iliyotolewa hii leo Novemba 2, 2024 inaonesha kuwa Waandishi 162 waliuwawa wakiwa kazini ambalo ni ongezeka la asilimia 38.

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Audrey Azoulay amearifu kuwa ongezeko hilo la mauaji linatia hofu, kwani hakuna hatua iliyochukuliwa katika karibu visa vyote vya mauaji.

Amesema kati ya nchi 75 ambazo UNESCO iliwasiliana nazo kwa ajili ya kupata idadi za Waandishi waliouwawa, 17 hazikutoa ushirikiano wowote na 9 zilikubali ombi hilo lakini hazikutoa majibu.

“Kati ya waandishi waliouwawa mwaka 2022 na 2023, 14 walikuwa wanawake na watano kati yao walikuwa kati ya umri wa miaka 15 hadi 24,” alibainisha Azoulay.

Hata hivyo, Azoulay ameyataka mataifa kuongeza juhudi za kuhakikisha wanaotenda vitendo hivyo vya kihalifu kwa kuwauwa Waandishi  wa Habari wanachukuliwa hatua.

Ruto ampa somo Kindiki, ataka ajiepushe na siasa za ukabila
TANZIA: Lala salama 'Tesa' Grace Mapunda