Rais wa Kenya, William Ruto amemtaka Naibu wake Prof. Kithure Kindiki kujiepusha na siasa za kikabila na maneno ya kuwqgawa Wakenya.
Ruto aliyasema hayo mara baada ya uapisho wa Prof. Kindiki uliofanyika Novemba Mosi 2024 katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya kuapishwa, Prof. Kindiki alisema atakuwa mtiifu na atahudumu nafasi hiyo kwa kumsaidia Ruto kuongoza Taifa la Kenya.
Prof. Kithure Kindiki aliapishwa rasmi kuwa Naibu Rais mpya wa Kenya, akichukua nafasi ya Rigathi Gachagua ambaye aliondolewa madarakani kwa tuhuma za kuwagawa Wakenya na kujilimbikizia mali.