Kiongozi wa kijeshi wa Guinea, Kanali Mamadi Doumbouya amejipandisha cheo cha juu ambapo anakuwa ni Jenerali.

Uamuzi huo umekuja ikiwa ni ishara ya kuchukua hatua za kuimarisha zaidi mamlaka ya vikosi vya kijeshi ambavyo tayari vina nguvu kubwa, huku wafuasi wake wakiendelea kumsihi agombee urais mara baada ya Jeshi kukabidhi Nchi kwa utawala wa Kiraia.

Doumbouya (43), aliingia madarakani kwa nguvu Septemba 2021 kwa kumpindua aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Alpha Conde, ambaye alimpa cheo Ukuu wa Kikosi Maalum cha Kijeshi kilichopewa jukumu la kumlinda mkuu  huyo wa nchi dhidi ya mapinduzi ya aina hiyo.

Hii inakuwa ni mara ya pili kuchukua hatua hiyo, kwani mapema Januari 2024 pia alijipandisha cheo na kuwa Kanali akiweka wazi kuwa Serikali yake ya kijeshi haitatimiza ahadi yake ya kurudisha mamlaka kwa raia.

Wanawake wakumbushwa kuzingatia malezi ya familia
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 3, 2024