Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi imefanya mafunzo maalum ya siku mbili yaliyolenga kuwajengea uwezo wakuu wa idara na vitengo pamoja na madiwani katika biashara ya hewa ya Kaboni.
Mafunzo hayo yamekwenda sambamba na kutembelea miradi mbalimbali iliyotekelezwa kwa kutumia fedha za biashara ya Kaboni, ikiwemo miradi ya afya, elimu na miundombinu iliyokuwa kikwazo kwa baadhi ya vijiji vinavyonufaika na mradi huo.
Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu amewataka washiriki kuwa mstari wa mbele katika suala la utunzaji wa mzingira.
Buswelu pia amewataka kuacha kushiriki katika uharibifu wa misitu kwa maslahi binafsi, huku Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Hamad Mapengo akiwaasa kufanya ufuatiliaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneo yao.