Kiongozi wa juu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei ameapa kulipiza kisasi dhidi ya Israel kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni yaliosababisha hasara kubwa.

Kauli hiyo ameitoa wakati maafisa wa chini yake wakizidi kutishia kuishambulia tena Israel, baada ya shambulizi la Oktoba 26, 2024 dhidi ya vituo vya kijeshi na maeneo mengine ya Iran, yalioua watu wasiopungua watano.

Kiongozi huyo wa Juu wa Iran pia ameonya kuwa Marekani na Israel zitakabiliwa na matokeo makubwa kwa vitendo vyao.

Kiongozi wa juu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.

“Vitendo vya adui havitasahaulika kwa wale wanaowakilisha taifa la Iran. Maadui ambao ni Marekani au utawala wa Kizayuni, wanapaswa kujua kwamba watapata majibu makali kwa kile wanachofanya dhidi ya Iran.”

Hata hivyo, Marekani imeionya Iran katika siku za karibuni dhidi ya kuishambulia tena Israel, huku maafisa wake wakisema Washington haitaweza kuizuia Israel ikiwa itashambuliwa tena.

credit@dw

Radi yauwa 14 wakiwa kwenye Ibada, miili haijatambuliwa
Biashara ya Kaboni: Madiwani Tanganyika wapewa darasa