Polisi Nchini Uganda, imethibitisha vifo vya watu 14 na 34 waliojeruhiwa kwa radi wakati walipokuwa kwenye maombi katika Kanisa la Zone 8, block 2, lililopo Kambi ya wakimbizi ya Palabek, kaskazini mwa Taifa hilo.
Kupitia chapisho la mtandao wa X lililotolewa hii leo Novemba 3, 2024 na Msemaji wa Polisi, Kituuma Rusoke ameeleza kuwa Kambi hiyo ya wakimbizi ipo Wilayani Lamwo na kwamba miili ya wahanga bado haijatambuliwa.
“Waathiriwa walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya maombi wakati mvua ilianza kunyesha mwendo wa saa 17:00 na radi ilipiga majira ya saa 5:30 usiku,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Polisi imesema hawajatambua uraia wa wahasiriwa lakini kambi hiyo na zingine katika eneo hilo huhifadhi wakimbizi kutoka Sudan Kusini na wengi wao walikuwa wamekimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoikumba nchi hiyo vilivyoanza mwaka 2011.