Maafisa wa Chama cha Walimu wa Shule za Sekondari na vyuo (KUPPET) wamemuomba Rais wa Kenya William Ruto awasaidie kuimarisha mazingira yao ya kazi pamoja na kuwaongezea mishahara na marupurupu.
Katika mkutano huo wa mwisho wa wiki, ukiofanyika katika Ikulu ya Nairobi KUPPET iliyongozwa na Mwenyekiti wake Omboko Milemba na Katibu Mkuu Akello Misori ilitoa msisitizo ju ya jambo hilo na kusema Serikali inapaswa kuwaangalia kwa jicho la ziada.
Kupitia taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo, Misori alidokeza kuwa chama hicho kilimweleza Rais kuhusu maslahi na hali ya mazingira ya kazi ya Walimu.
“Tuliomba Rais ahakikishe kuwa TSC inapata fedha zaidi ili kuwapandisha walimu 130,000 vyeo, kuajiri walimu zaidi na kutathmini marupurupu mbalimbali ya walimu,” alisema Bw Misori.
Ombi hilo linakuja ikiwa ni baada ya Chama hicho kulalamika kuwa Tume ya Kuwaajiri Walimu (TSC), haijakuwa ikiwasilisha makato ya Wanachama kwa muungano huo kwa kipindi cha miezi mitatu na hivyo kukosa daraja la luwafikia watendaji wa juu ili kumaliza kero zao.