Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amekabidhi eneo la ekari 8 lililopo Makatanini Wilayani Babati Mkoani Manyara kwa Taasisi ya Mwinyi Baraka Islamic Foundation, kwa ajili ya huduma za kidini ya imani ya Kiislamu.

Akiongea baada ya kukabidhi eneo hilo, Sendiga amesema litatumika kwa uwekezaji mkubwa katika Mkoa wa Manyara, huku akiwakaribisha Wananchi wanaotaka kuwekeza Mkoani Manyara wafike kuchangamkia uwepo fursa nyingi.

Amesema, uwekezaji huo utaisaidia kuwainua Vijana kwa kujifunza fani mbalimbali za kujiajiri kufuatia kuwepo kwa changamoto ya ajira kwa wengi wao,hivyo uwekezaji huo utasaidia kupunguza ongezeko la wategemezi.

Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Taifa, Sheikh Issa Othman Issa, ameupongeza uongozi wa Mkoa kwa kukubali uwekezaji huo, ambapo amesema mbali na Msikiti wataweka huduma mbalimbali za kijamii.

 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Kaganda amesema wamefurahishwa na uwekezaji huo huku Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Abdarahman Kololi akiishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na taasisi za kidini.

 

Maskini Neymar maisha yake ya soka ndo basi tena
NBC: Fountain Gates yampasua kichwa Minziro