Serikali Nchini Equatorial Guinea, imesema itawafukuza kazi Maafisa na Watumishi wote wa Umma ambao ni miongoni mwa Wanawake zaidi ya 400, waliorekodiwa wakifanya mapenzi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Upelelezi wa Fedha la Nchi hiyo – ANIF, Baltasar Ebang Engonga (54).
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mangue kufuatia kitendo hicho cha Ebang ambaye tayari amekamatwa kwa kujirekodi akiwa anafanya mapenzi na Wanawake haowakiwemo Wake za Watu, Mdogo wa mke wa Kaka yake, Binadamu yake.
Wengine ni Dada wa Rais wa Equatorial Guinea, Mke wa Mkuu wa Ulinzi wa Rais wa Nchi hiyo, Mke wa Mwanasheria Mkuu wa Nchi hiyo na Mtoto wa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Nchi hiyo Mke wa Mlinzi wake, Mke wa Mchungaji wake na Wake wa baadhi ya Mawaziri wa Nchi hiyo.
Aidha katika picha hizo mjongeo, pia wamo Mke wa Mjomba wake ambaye ni Mjamzito, Marafiki 15 wa Mdogo wake wa kike na wengineo mbalimbali na inadaiwa kuwa wote waliridhia video hizo kurekodiwa.