Kinyang’anyiro cha kuingia katika Ikulu ya White House kati ya mgombea wa chama cha Republican, Donald Trump na mgombea wa chama cha Democratic Kamala Harris kinaonekana kuwa kikali, huku taifa hilo likisubiri kwa hamu matokeo ya uchaguzi huo mkali zaidi katika historia ya Marekani.
Matokeo ya uchaguzi huo, yataamua iwapo yatamuweka madarakani Harris na kuwa Mwanamke wa kwanza katika historia ya kuliongoza taifa hilo lenye nguvu duniani au kumrejesha Trump madarakani.
Mpaka sasa matokeo ya awali yanaonesha kuwa mgombea wa chama cha Republican Donald Trump amepata kura 198 za wajumbe wa Kamati Maalum ya uchaguzi nchini Marekani, ambayo inamchagua Rais maarufu kama Electoral College, na mgombea wa chama cha Democratic, Kamala Harris amepata kura 109 za Electoral College.
Trump ameshinda katika majimbo ya 14 yakiwemo ya, Indiana, Florida, Alabama, South Carolina, Texas, na jimbo la Nebraska, Huku Harris akishinda kwenye majimbo 11 yakiwemo ya Maryland, New York na Mississippi.
Ushindi wa Trump Florida ni wa mara ya tatu mfululizo kwani Mgombea wa urais wa chama cha Democratic hajawahi kushinda kwenye jimbo hilo, tangu Barack Obama aliposhinda mwaka 2012 na mshindi anahitaji kupata kura 270
huku kila mgombea akihitaji kupata kura 270 za Electoral College kati ya 538 zinazohitajika ili kushinda.
Katika matokeo ya kura za Wananchi wa kawaida zilizohesabiwa hadi muda huu, Harris kapata kura asilimia 46.3, na Trump asilimia 52.6 na matokeo ya hayo yanaweza kujulikana punde tu baada ya siku ya uchaguzi au yanaweza kuchukua wiki kadhaa hadi yatakapothibitishwa.