Manchester United na Chelsea wanamuwania Viktor Gyokeres, Real Madrid wana nia ya kumnunua Trent Alexander-Arnold mwezi Januari, Al-Hilal huenda wakafuta kandarasi ya Neymar na kumnunua Cristiano Ronaldo.
Manchester United na Chelsea wataongoza kinyang’anyiro cha kumnunua mshambuliaji wa Uswidi na Sporting Viktor Gyokeres,26, msimu ujao. (Stra)
Gyokeres atauzwa kwa takriban euro milioni 63 msimu ujao – euro milioni 20 chini ya kifungu chake cha kutolewa. (Telegraph – usajili unahitajika)
Manchester United pia wanamfuatilia kiungo wa kati wa Bayern Munich Mjerumani Leon Goretzka mwenye umri wa miaka 29. (Florian Plettenberg)
Real Madrid wana nia ya kumnunua beki wa Liverpool Muingereza Trent Alexander-Arnold, 26, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu (Marca – kwa Kihispania).
Lakini Liverpool hawako tayari kumuuza mchezaji yeyote wa kikosi cha kwanza mwezi Januari. (Football Insider)
Al-Hilal wanafikiria kusitisha kandarasi ya mshambuliaji wa Brazil mwenye umri wa miaka 32 Neymar mnamo Januari na badala yake wamnunue mshambuliaji wa Ureno wa klabu ya Saudi ya Al-Nassr, 39, Cristiano Ronaldo. (Sport – kwa Kihispania)
Arsenal, Liverpool na Tottenham wanavutiwa na kiungo wa kati wa Eintracht Frankfurt wa Uswidi Hugo Larsson, 20. (Caught Offside)
Crystal Palace wanapanga kuwasilisha dau la pauni milioni 20 la kumnunua kiungo wa kati wa Sunderland na England chini ya umri wa miaka 18 Chris Rigg mwezi Januari. (Sun)
Everton wameonyesha nia ya kutaka kumsajili beki wa Brighton wa Ghana Tariq Lamptey kwa uhamisho wa bila malipo mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu. (Africa Foot – kwa Kifaransa)
Muungano unaoongozwa na mfanyabiashara wa Marekani Steve Rosen unakaribia kukamilisha ununuzi wa klabu ya Sheffield United kwa kima cha mauni milioni 105. (Telegraph – usajili unahitajika)
Tottenham wanafikiria kumnunua winga wa Nottingham Forest na Uingereza Callum Hudson-Odoi, 23. (Football Insider)
AC Milan, Inter Milan na Napoli wanavutiwa na mlinzi wa Arsenal Jakub Kiwior, 24, lakini The Gunners watazingatia tu kumruhusu kuondoka kabisa kwa ada, wala sio kwa mkopo. (Tutto Mercarto – kwa Kiitaliano)
Brentford ni miongoni mwa klabu zinazovutiwa na mshambuliaji wa Celta Vigo na Ugiriki Anastasios Douvikas, 25. (Mundo Deportivo – kwa Kihispania)
West Ham watatathmini umpya nafasi yakocha Julen Lopetegui iwapo The Hammers wanaotatizika watapoteza mechi ya nyumbani dhidi ya Everton Jumamosi hii.