Tabora United imewashangaza mashabiki wa soka kwa ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Yanga.Ni Often Chikola aliyekuwa wa kwanza kupachika bao dakika ya 25 akimalizia pasi murua kutoka kwa Yacouba Sogne.Dakika ya 45+4 Offen Chikola alipachika bao la pili akimalizia pasi ya Yacouba Sogne na kuufanya mchezo kwenda mapumziko Tabora United wakiongoza kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili Kocha wa Yanga alifanya mabadiliko kwa kuwatoa Kenedy Musonda,Aziz ki ,Pacome kisha nafasi zao kuchukuliwa na Clement Mzize,Chama na Prince Dube. Mbali na nyota hao kuingia Tabora waliendelea kuleta ushindani na dakika ya 78 Nelson Munganga alipachika bao la tatu. Dakika ya 90+5 Yanga walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Clement Mzize.

Kwa mara ya kwanza mashabiki wa Yanga waliishuhudia timu yao ikicheza na washambuliaji watatu ambao ni Mzize ,Dube na Baleke. lakini kukosekana kwa  Job,Bacca ,Boka na Yao katika mchezo huo kulipelekea safu ya ulinzi kuwa dhaifu na kupelekea Yanga kupoteza mchezo huo.

Aziz Andambwile ,Mwamnyeto ,Kibabage na Denis Nkane walishindwa kufanya  kile walichotumwa na mwalimu baada ya kufanya makosa ya kujirudia na kusababisha dhahma ya mabao 3.

Matokeo hayo yanawafanya Tabora United kufikisha alama 17 wakishika nafasi ya 6 kwenye mechi 11 walizocheza . Yanga wameendelea kusalia nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 24 kwenye michezo 10 waliyocheza mpaka sasa.

Dkt. Biteko aiwakilisha Nchi uapisho Rais wa Botswana
Manchester United yarejea kwa kishindo Europa