Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Richard Abwao amesema Dereva wa gari aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T 562 DGG aliyesababisha ajali iliyouwa Watu 14 kujeruhi wengine Tisa alikimbia baada ya tukio.

Ajali hiyo ilitokea katika Kijiji cha Mwansengo kilichopo Kata ya Itobo Wilayani Nzega Mkoani Tabora, na kusababisha vifo vya Wanaume wanane, Wanawake wanne, Watoto wawili na majeruhi tisa, baada ya Gari hiyo kugonga Gari jingine aina ya Fuso Mitsubishi lenye namba za usajili namba T 361 CSB.

 

Amesema, “Novemba 07, 2024 majira ya saa mbili na dakika ishirini Kuna ajali imetokea katika barabara ya Itobo-Bukene katika kijiji cha Mwansengo Kata ya Itobo ambapo Dereva wa Gari lenye namba za usajili T 562 DGG Toyota Hiace likendeshwa na dereva ambaye hajafahamika Jina.”

Kamanda Abwao amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva ambaye amekimbia alipokuwa akijaribu kulipita Lori lililokuwa mbele yake na kushindwa kulimudu gari alilokuwa akiendesha hivyo kuligonga Lori upande wa kulia kwa nyuma na kuingia chini ya uvungu wa Lori.

Ustawi wa Taifa: Viongozi timizeni majukumu yenu - Mchengerwa
Dkt. Biteko aiwakilisha Nchi uapisho Rais wa Botswana